Description
Laura Fair ni Profesa wa historia na anafundisha Michigan State
University, Marekani. Aliishi Zanzibar miaka kadha alipofanya utafiti
kwa ajili ya kitabu chake cha kwanza: Pastimes and Politics: Culture,
Community and Identity in Post-abolition Urban Zanzibar, 1890-1945.
Katika kitabu hicho anaeleza jinsi ambavyo watumwa walidai uhuru
wao kutoka kwa mabwana wao na vile walivyojaribu kudai haki zao
kutoka kwa watawala wapya, Waingereza. Baadaye alifanya utafiti
visiwani na Tanzania bara kuhusu historia ya sinema na anategemea
kuchapisha kitabu kingine kuhusu sinema hivi karibuni.
Kama maprofesa wengi wa enzi za nyuma wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Profesa Fair ni mfugaji pia. Huko Marekani anafuga kuku na
kondoo bila matumizi ya dawa (kiasilia) na pamoja na mtoto wake Sabri
wanalima takriban vyakula vyao vyote. Njoo Marekani, uwatembelee
huko mashambani